Moja ya njia/ namna ya kutengeneza pesa pesa mtandaoni nnaotumia ni Affiliate Marketing, na ina nguvu kuliko mtu anavyoweza kufikiri.
Sio kila mtu anaweza kumudu kuwa na store, na najua wengi wameanza kutafuta riziki ao kwa kuanza kutengeneza blog ili baadae waje waweke maangazo ya Adsense.
Swala la Adsense ndio swala linalofanya blog za waanzania zinazozidi kujazana kila siku zisiwe productive. Hivi karibuni niliona notice kuwa blog zinapaswa kulipa pesa serikalini na kusajiliwa ili kuendelea kutumika (Kinyume na hapo zitawaweka kwenye matatizo)
Swala Hili limepokelewa vibaya, haswa na ma bloggers wadogo ila wameshindwa kujiuliza ni kwanini serikali imeamua kuweka kiasi husika kwa majukwaa na channel kadhaa za youtube. Najua blog nyingi haziko targetted zilizo tagetted ni haswa za habari na siasa.
Hata kama hauko targetted, mambo yakianza kubana hivi ujue kuna fursa/potential wameona mpaka kufikia atua ya kuanza kuichkulia kama biashara na ni kazi ya nguvu kazi kuambua potential gani imeonwa na serikali.
Najua hawajaweka pricing husika wakijua blog ziko monetised na matangazo ya Adsense(Adsense Hairuhusu Monetisation Kwa Content Za Kiswahili) Na hata wanekuwa wanaruhusu bado ni pesa ndogo sana inayopokelewa na bloggers kupitia Adsense(Na Masharti Yao Ni Magumu) So Kuna Potential Nyingi tu kwenye blogging ambazo zikitambulika zitaingizia vijana pesa, wataweza kumudu makato ya serikali na kuingizia serikali mapato na kujinufaisha wenyewe pia.
Moja ya Njia Nzuri na Imara ya Kuengeneza Kiasi Husika Cha Pesa Ni Affiliate Marketing. Ni biashara ninayoianya tofauti na drpshipping na inalipa ukiifanya vizuri..Na madhumuni ya kuleta thread hii ni kujaribu kutoa tongotongo.
Saa nyingine naandika, nikiwa sijui wangapi watasoma ila kwa hao hao watakao soma, ikimsaidia mmoja basi sijapoteza mda wangu!
Kwa Hiyo Affiliate Marketing Nini?
Kwa kiswahili kisicho fasaa na ninacho ona ni rahisi kuelewa,
Affiliate Marketing Ni Njia ya Kutengeneza Pesa Ambapo Mmiliki Wa Bidhaa anakulipa Kamisheni ya asilimia mliyokubaliana, endapo mtu akinunua bidhaa husika kupitia Affiliate Link Yako.
Sana sana bidhaa zinazo husiswa hapa huwa ni digital kama Podcast, Webinar, Software, Course, E-Book na hata Web Tools...Hii ina maana hakuna shipping wala billing kama dropshipping hivyo ni flexible kufanyika kokote.
Ohh! Sasa Inafanyaje Kazi?
Katika Makala Hii, Nitazungumzia Kuengeneza Pesa Kwa Kutumia Affiliate marketing na Blog Kwa pamoja japokuwa Kuna Njia Kadhaa Unazoweza Tumia, Nimeelezea Kwenye Blog Yangu.
Kwenye Affiliate marketing Huwa Kuna, Wewe(Affiliate), Dalali(Advertiser) na Mmiliki wa Bidhaa.....Dalali sio lazima awepo kwenye sstem maana mmilikiwa bidhaa anaweza kuwa bado ana affiliation program anakoweza ku manage affiliates wake.
Utakacho hitaji ni blog ya kingereza ambako utaandika specific content, Labda Self-Help, Love & Relationships, Entrepreneurship, Au Gaming..>Sikushauri kuingia kwenye habari nk.
Baada ya Kufanya hivyo, Tengeneza Audience, Njia ahisi ya kufanya hivyo ni kwa kufanya SEO(Search Engine Optimization) ambayo itafanya blog yako kuonekana google. Ukianza kupata visiors wengi ambao watakuwa wakrudi mara kadhaa, sasa utakuwa tayari kuenda kwenye hatua inayofuata.
Kujiunga na Affiliate Program
Zipo Affiliate Program Nyingi, ila ambayo imenisaidia kutengeneza pesa ya maana, tofauti na(Dropshipping) ni JVZoo.
Ni rahisi na bure kujiunga, utakuwa approved in 5 Minutes na unaweza pokea malipo kupitia PayPal au Wire Transfer(Bank)...najua Tanzania haturuhusiwi kupokea pesa kupitia PayPal, ila nakusauri kufanya mbinu ya kumiliki account ya PayPal inayoweza kutoa hela maana malipo yatakuwa Instant. Na Wire Transfer Inachukua karibia siku 30. Ni nyingi sana!
Mfano mmi nimetengeneza Visual Credit Card mtandaoni, ambayo nmelink na account yangu ya bank...Nimeitumia ku register PayPal kama citizen wa US na JVZoo wananilipa kwa PayPal...then natuma pesa yangu kwenda Payoneer ambako nimelink na Bank..Hiyo Visual Card ni kwa ajili a Verification.
Kama Una Ndugu Njee anaweza kukusajilia account huko, pesa ikishatka ni rahisi kuipata.JVZoo wanalipa automaically ukifika $100 na baada ya hapo utaanza kuamua kupata Auo-Payment au Manual.
Ok. Natengenezaje Pesa Sasa?
Ni rahisi, tuchukulie kuwa una blog ya Mahusiano labda unasaidia wanaume kupata confidence ya ku approach wadada, unaweza afuta course kutoka JVZoo inayohusiana na iyo mada, kisa kupaa affiliate link.
Sasa kipindi unaadika kwenye makala yako unaweza sugest course husika au kitabu..Kama tayari una audience inayopenda kufuatilia makala zako, baso kuna chance kubwa kuwa watanunua! Hata kama awakufuatilii..ila kama ni wengi 40% itabofya link na 10-15% Itanunua!
Okey, mfano bidhaa tuliyo promote inauzwa $45, na kamisheni yako ni 40% umepata watu kumi wanao soma blog yako wakanunua...hapo una faida ya $180 kwa siku/wiki!
Ukipata watu 50 watakao nunua kupitia link yako ni $900 na kadiri watu wanavyoongezeka nipo mambo yanazidi uwa matamu!
Blog zangu zote za kiswaili hazina matangazo wala afiliaion maana lengo lake ni kusadia wengine wawe kama mmi....Ila blog za kingereza ni kutatua mataizo na ukifanya affiliaion unaweza benefit....Step ya kwanza kumbuka ni kutafuta audience na unaweza fanya SEO....(nimeengeneza video kuhusu SEO kwenye channel yangu)
Wapo watanzania wanaoengeneza pesa nefu maana stats za serikali labda zimewaonesha kuja kufikia kuamua kuweka regulations, unaweza kuwa mmoja wao ili hata ukisikia hizo prcing na makato au kodi usistke ka mimi.
Hii ndo screenshot yangu ya JVZoo kwa Leo Mwezi September, na withdraw kila siku na siamini kwenye kujaza blog na matangazo.